Monday, December 5, 2022

TOP TEN (KUMI BORA) MASHIRIKA NA MAKAMPUNI BINAFSI YANAYOLIPA MISHAHARA MIKUBWA

 1. WALTER REED FOUNDATION

2. USAID PROJECTS

3. TBL
4. SBL
5.TCC
6. TWIGA CEMENT
7. SONGWE CEMENT
8. ALLIANCE ONE TOBACCO
9. COCA COLA
10. TOYOTA TANZANIA

Tuesday, November 29, 2022

President ajaye atoke Mbeya? Je nini maoni yako?

 Kama mjuavyo Mbeya ni kama Israel ya Tanzania, au Makkah kwa Waislamu! Vitu vingi vizuri na bora vinatoka Mbeya.

Kanisa la kwanza la kilokole lilianzia Ighale Mbeya, asilimia tisini na tisa ya wachungaji wenye upako na viwango wanatoka Mbeya, Maaskofu karibu robo tatu nchini wanatoka Mbeya, waimbaji wakubwa Tanzania wa dini wanatoka Mbeya ukianza na Daniel Mwasumbi, Efraim Mwansasu r.i.p, mpaka kizazi cha akina Boni Mwaitege wote wametoka Mbeya!

Mbeya ni mji mtakatifu sana kwa historia, ardhi yake imebarikiwa ni kama Denmark au Australia, muda wote ni kubichi. Watu wengi huwa wanashangaa uwingi wa makanisa Mbeya sababu ni kwamba Mbeya ndiyo Israel ya Tanzania, ni mji wa ibada.

Askofu Moses Kulola alianzia utume wake Itende Mbeya na Askofu Lazaro pia alilazimika kuanzia Mbeya kisha wakaicapture nchi kwa vuguvugu la wokovu!

Wasomi wanaotokea Mbeya ni material kwelikweli, kwa sasa iwe zamu ya Mbeya, Rais ajaye atoke Mbeya. Mtakuja kunishukuru hapa.

Haya NI maoni ya Mganguzi kutoka jamii forum

Sunday, November 13, 2022

CHUPI ZA UPAKO ZAWASHANGAZA WAKRISTO (Soma kisa hiki kikusaidie)

Jana nilimsindikiza shemeji  kwa nabii. Kilichompeleka yeye ni shida na changamoto za mahusiano yake. Mume mlevi, mume Malaya Kama mbwa, mume bahili, hajali ndoa Wala familia. Hajali ndugu zake Wala wa mkewe. Mume mgumu Kama ndevu za gaidi wa Mkuranga.

Rafiki yangu huyu aliniomba niandamane naye kwa nabii ili aniangalizie Mambo yangu, kwani tangu kipindi Cha Corona Biashara zangu zimeyumba Sana na hata shamba langu la nyoka  ambalo ndilo lilikuwa likiniingizia fedha za kigeni Sasa najihisi kana kwamba linaweza kunishinda kabisa ku operate.

Sasa kila mtu aliingia kwa awamu yake chumbani kwa nabii. Mimi ndiye niliyeanza na Kisha shem akafuatia. Nabii alikuwa mchangafu akanitia moyo kuwa hata kampuni kubwa Ulaya zimeanguka, nijipe Moto nitainuka Tena.

https://youtu.be/9VqdA0_DTNE

Akaniombea nikatoka, akaingia shemeji . huko ndani alikaa zaidi ya saa moja, akatoka nje akaniuliza una laki moja hapo unipe ntakurejeshea nyumbani? Nikamjibu cash Nina 75'000/ akasema nipe hizohizo, na Kama unayo balance kwenye simu rusha kwa namba hiii ya nabii. Nikamrushia.

Shem akaingia ndani ambako Sasa alikaa Kama dakika Saba Kisha akatoka nje. Safari ya kuelekea kwenye gari ikaanza, ndipo akaanza kunipa mchapo.

Nabii anatoa chupi za upako ambazo zinasaidia Kama mume hatulii, una ugumba etc. Chupi ni za Holland Wax na unaweza jipatia kwa kadiri utakavyo.

Bei ya kila moja ni laki unusu.

TAHADHARI :

Dada zangu sio kila nabii katoka kwa BWANA, muwe makini vinginevyo mtaibiwa sana

@Jr James (Facebook)

MIMI SITAKUPA USHAURI WOWOTE MSOMAJI WANGU BALI SOMA MANENO YA MUNGU YAKUSAIDIE KISHA UFANYE MAAMUZI YAKO BINAFSI KUCHAGUA UPANDE WA KUSMAMIA IMANI YAKO. NAKUOMBEA SANA MUNGU AKUTIMIZIE HITAJI LA MOYO WAKO AMEN

Tuesday, November 8, 2022

Zifahamu Nyimbo za Angela Chibalonza alizoimba kabla hajafahamika

Mwanamuziki WA nyimbo za Injili kutoka Congo aliyepata umaarufu mkubwa Sana miaka iliyopita aitwaye MAREHEMU Angela Chibalonza, aliwahi kuimba nyimbo KADHAA nzuri Sana kabla ya kufahamika kwenye Tasnia ya Muziki WA Injili.

  Mwanadada huyo ambaye Kwa sasa ni MAREHEMU aliimba nyimbo ZIFUATAZO ambazo NI miongoni MWA nyimbo ambazo yumkuni hukuwahi kuzifahamu. Nyimbo hizo zipo YouTube na mitandao mingine ya kidigitali ambapo nyimbo za Injili hupatikani.


Nyimbo hizo ni;

1. Inua Moyo wangu.  

    https://youtube.be/kuR5fjJZ8P8

2. Wamwendea (TENZI)

https://youtube.be/GFvfQCQhHtl

3. Ndio dhamana 

4. Tuonane bandarini (TENZI)

5. Yesu unipendaye (TENZI)

6. Mteteeni Yesu (TENZI)


Zipo Kwa mfumo WA video na audio ingia YouTube andika Angela Chibalonza na  utazipata nyimbo zake zote huko.

Edelea kubarikiwa na kuhudumiwa na taarifa mbalimbali za Gospo hapa kwenye blog yetu. 

Tunakupenda











Sunday, July 16, 2017

GOSPEL SINGERS AND A GOSPEL COMEDIANS

WAIMBAJI NA WAIGIZAJI KOMEDI KWA UPANDE WA INJILI


It has been an amazing story that, a gospel singer in Tanzania Beatrice Kitauli, appears to have showing a talent of acting comedy. For that opportunity, she continue to include that talent into serving God of which she with her other 3 fellow gospel singers are now preparing a Gospel comedy named GazuKita Gospel Comedy which will be of conveying God's word via comedy.

With this, she with the team explains that, everything will be settled at least by August 2017 of which different sessions of their Gospel comedy will be appearing in different social media networks and other media as it may apply.

Other members who will be joining her are Gazuko Junior who is also a Gospel singer and Media presenter, Moses Simkoko who is also a gospel singer and a businessman, and Maria Richard who is an actress.
They all emphasize that, different gospel stakeholders should not worry because this is not a new means of conveying God's word , but it is just like other means like singing, teaching, preaching and other means. So every one is encouraged to enjoy while "eating spiritual food" (God's word)

They also thanked all who are continuing to support them by advising them positively and negatively, financially and spiritually 


Monday, April 3, 2017

"KWA TANZANIA UELEWA KUHUSU TUZO ZA GOSPO TUPO NYUMA"; BEATRICE KITAULI ASEMA..SOMA HAPA ZAIDI








Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye pia alishinda tuzo za xtreem awards Kenya mwaka 2015/2016 (tuzo ya most promising artist yaani mwimbaji anayekuja kwa kasi) amefanikiwa tena kuingia kwenye tuzo za Gospel awards zilizoandaliwa kufanyika mapema mwezi April 2017.
Beatrice Kitauli amesema kwamba, kuchaguliwa kwake kwenye tuzo hizo tena kwa vipengele  viwili tofauti (two categories) kwa wakati mmoja kwake ni "NEEMA" Ameendelea kufafanua kwamba amefarijika kuona kuwa Mungu anawatumia watu kutambua kazi wanazofanya watumishi/waimbaji/watangazaji/wachungaji n.k.

Beatrice anasema; "Unajua, Mungu hajawai kushuka akashikika na akaonekana kwa macho kisha akampongeza mtumishi wake kwa kumpa zawadi kama kitenge, pesa, maua n.k huo ni mfano tu nasema. Huwa Mungu anatumia watumishi wake waandae tuzo kama hizi ili watutie moyo na kutambua jitihada zetu katika kuinjilisha hapa Duniani. Japo tuzo kubwa tutapata mbinguni lakini tunatiana moyo ili kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii Zaidi.

Beatrice Kitauli anaendelea kusema:
"Kwa Tanzania bado uelewa kuhusu maswala ya Tuzo za gospo tupo nyumba ndio maana wengi sana wanaibuka na kuwakatisha wenzao tamaa. Ila tukiendelea kuelimishana na kutiana moyo tutafika mbali Zaidi. Hata kama uko kiroho Zaidi lakini sote tunaishi duniani tukiwa na mwili wa nyama. Hivyo kutambua, kuthamini na kuheshimu huduma za wenzetu ni jambo zuri sana la upendo."

Beatrice anaendelea kufafanua kwamba;
Uelewa mdogo kwa watanzania kuhusu tuzo za Gospo ndio unasababisha wadau wengi wa gospel wanyooshe vidole kuhoji uhalali wa waimbaji wengine kuwepo kwenye tuzo mbalimbali. Na hivyo ni Neema na hekima ya Mungu tu inahitajika na elimu Zaidi inatakiwa itolewe na waandaji kwa wahusika ili malalamiko yapungue.

Beatrice anamalizia kwa kusema; Nimeona tuzo chache sana za gospo zikiandaliwa na watanzania wachache waliodhubutu, wengi wanaoandaa ni Wakenya na nchi zingine chache ambazo wamepiga hatua kwenye jambo hili... Me nawaomba wadau wa gospo tushirikiane tushikamane kwa upendo maana hapo ndipo tutainjilisha kwa mafanikio kama alivyotuagiza Baba tuje tuihubiri injili ulimwenguni kote.......

Kwa kila jambo yatupasa kushukuru
Zaburi 136:1-4

Asante Mungu wa mbinguni
Asante sana wadau wa gospel music na watu wote
Asante sana Gospo Media

Kwa nyimbo alizoimba Beatrice Kitauli zinapatikana linki ifuatayo youtube; http://bit.ly/2g27EFW
Facebook: Beatrice Kitauli
Instagram: Beatrice Kitauli
Twitter: Beatrice Kitauli
Watsap: +255 757 830 451

Thursday, March 23, 2017

PICTURES FOR DAY 3 CRUSADE AT KIVULE (MKUTANO WA INJILI KIVULE SIKU YA 3)




















Habari ya leo.
Endele kuambatana name kwenye matukio yoote yanayohusu injili ya Yasu

Hizi ni picha za mkutano siku ya tatu pale Kivule Kitunda ambapo mkutano
unaendelea hadi tarehe 26.03.2017

Mtumishi wa Mungu Joel Kyando anaendelea kuhubiri akiambatana na waimbaji Beatrice Kitauli, Happy Samson, Joshua Kyando, Bahati Simwiche, Kibonge wa Yesu na wengine weengi.
Mungu anaendelea kuonekana kwa namna ya tofauti na walio wengi wanafanywa kuwa wana

Wote mnakaribishwa. Wagonjwa na wenye shida mbalimbali waletwe ili waombewe

Asante