Tuesday, November 29, 2022

President ajaye atoke Mbeya? Je nini maoni yako?

 Kama mjuavyo Mbeya ni kama Israel ya Tanzania, au Makkah kwa Waislamu! Vitu vingi vizuri na bora vinatoka Mbeya.

Kanisa la kwanza la kilokole lilianzia Ighale Mbeya, asilimia tisini na tisa ya wachungaji wenye upako na viwango wanatoka Mbeya, Maaskofu karibu robo tatu nchini wanatoka Mbeya, waimbaji wakubwa Tanzania wa dini wanatoka Mbeya ukianza na Daniel Mwasumbi, Efraim Mwansasu r.i.p, mpaka kizazi cha akina Boni Mwaitege wote wametoka Mbeya!

Mbeya ni mji mtakatifu sana kwa historia, ardhi yake imebarikiwa ni kama Denmark au Australia, muda wote ni kubichi. Watu wengi huwa wanashangaa uwingi wa makanisa Mbeya sababu ni kwamba Mbeya ndiyo Israel ya Tanzania, ni mji wa ibada.

Askofu Moses Kulola alianzia utume wake Itende Mbeya na Askofu Lazaro pia alilazimika kuanzia Mbeya kisha wakaicapture nchi kwa vuguvugu la wokovu!

Wasomi wanaotokea Mbeya ni material kwelikweli, kwa sasa iwe zamu ya Mbeya, Rais ajaye atoke Mbeya. Mtakuja kunishukuru hapa.

Haya NI maoni ya Mganguzi kutoka jamii forum

No comments:

Post a Comment