Monday, April 3, 2017
"KWA TANZANIA UELEWA KUHUSU TUZO ZA GOSPO TUPO NYUMA"; BEATRICE KITAULI ASEMA..SOMA HAPA ZAIDI
Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye pia alishinda tuzo za xtreem awards Kenya mwaka 2015/2016 (tuzo ya most promising artist yaani mwimbaji anayekuja kwa kasi) amefanikiwa tena kuingia kwenye tuzo za Gospel awards zilizoandaliwa kufanyika mapema mwezi April 2017.
Beatrice Kitauli amesema kwamba, kuchaguliwa kwake kwenye tuzo hizo tena kwa vipengele viwili tofauti (two categories) kwa wakati mmoja kwake ni "NEEMA" Ameendelea kufafanua kwamba amefarijika kuona kuwa Mungu anawatumia watu kutambua kazi wanazofanya watumishi/waimbaji/watangazaji/wachungaji n.k.
Beatrice anasema; "Unajua, Mungu hajawai kushuka akashikika na akaonekana kwa macho kisha akampongeza mtumishi wake kwa kumpa zawadi kama kitenge, pesa, maua n.k huo ni mfano tu nasema. Huwa Mungu anatumia watumishi wake waandae tuzo kama hizi ili watutie moyo na kutambua jitihada zetu katika kuinjilisha hapa Duniani. Japo tuzo kubwa tutapata mbinguni lakini tunatiana moyo ili kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii Zaidi.
Beatrice Kitauli anaendelea kusema:
"Kwa Tanzania bado uelewa kuhusu maswala ya Tuzo za gospo tupo nyumba ndio maana wengi sana wanaibuka na kuwakatisha wenzao tamaa. Ila tukiendelea kuelimishana na kutiana moyo tutafika mbali Zaidi. Hata kama uko kiroho Zaidi lakini sote tunaishi duniani tukiwa na mwili wa nyama. Hivyo kutambua, kuthamini na kuheshimu huduma za wenzetu ni jambo zuri sana la upendo."
Beatrice anaendelea kufafanua kwamba;
Uelewa mdogo kwa watanzania kuhusu tuzo za Gospo ndio unasababisha wadau wengi wa gospel wanyooshe vidole kuhoji uhalali wa waimbaji wengine kuwepo kwenye tuzo mbalimbali. Na hivyo ni Neema na hekima ya Mungu tu inahitajika na elimu Zaidi inatakiwa itolewe na waandaji kwa wahusika ili malalamiko yapungue.
Beatrice anamalizia kwa kusema; Nimeona tuzo chache sana za gospo zikiandaliwa na watanzania wachache waliodhubutu, wengi wanaoandaa ni Wakenya na nchi zingine chache ambazo wamepiga hatua kwenye jambo hili... Me nawaomba wadau wa gospo tushirikiane tushikamane kwa upendo maana hapo ndipo tutainjilisha kwa mafanikio kama alivyotuagiza Baba tuje tuihubiri injili ulimwenguni kote.......
Kwa kila jambo yatupasa kushukuru
Zaburi 136:1-4
Asante Mungu wa mbinguni
Asante sana wadau wa gospel music na watu wote
Asante sana Gospo Media
Kwa nyimbo alizoimba Beatrice Kitauli zinapatikana linki ifuatayo youtube; http://bit.ly/2g27EFW
Facebook: Beatrice Kitauli
Instagram: Beatrice Kitauli
Twitter: Beatrice Kitauli
Watsap: +255 757 830 451
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment