Sunday, November 13, 2022

CHUPI ZA UPAKO ZAWASHANGAZA WAKRISTO (Soma kisa hiki kikusaidie)

Jana nilimsindikiza shemeji  kwa nabii. Kilichompeleka yeye ni shida na changamoto za mahusiano yake. Mume mlevi, mume Malaya Kama mbwa, mume bahili, hajali ndoa Wala familia. Hajali ndugu zake Wala wa mkewe. Mume mgumu Kama ndevu za gaidi wa Mkuranga.

Rafiki yangu huyu aliniomba niandamane naye kwa nabii ili aniangalizie Mambo yangu, kwani tangu kipindi Cha Corona Biashara zangu zimeyumba Sana na hata shamba langu la nyoka  ambalo ndilo lilikuwa likiniingizia fedha za kigeni Sasa najihisi kana kwamba linaweza kunishinda kabisa ku operate.

Sasa kila mtu aliingia kwa awamu yake chumbani kwa nabii. Mimi ndiye niliyeanza na Kisha shem akafuatia. Nabii alikuwa mchangafu akanitia moyo kuwa hata kampuni kubwa Ulaya zimeanguka, nijipe Moto nitainuka Tena.

https://youtu.be/9VqdA0_DTNE

Akaniombea nikatoka, akaingia shemeji . huko ndani alikaa zaidi ya saa moja, akatoka nje akaniuliza una laki moja hapo unipe ntakurejeshea nyumbani? Nikamjibu cash Nina 75'000/ akasema nipe hizohizo, na Kama unayo balance kwenye simu rusha kwa namba hiii ya nabii. Nikamrushia.

Shem akaingia ndani ambako Sasa alikaa Kama dakika Saba Kisha akatoka nje. Safari ya kuelekea kwenye gari ikaanza, ndipo akaanza kunipa mchapo.

Nabii anatoa chupi za upako ambazo zinasaidia Kama mume hatulii, una ugumba etc. Chupi ni za Holland Wax na unaweza jipatia kwa kadiri utakavyo.

Bei ya kila moja ni laki unusu.

TAHADHARI :

Dada zangu sio kila nabii katoka kwa BWANA, muwe makini vinginevyo mtaibiwa sana

@Jr James (Facebook)

MIMI SITAKUPA USHAURI WOWOTE MSOMAJI WANGU BALI SOMA MANENO YA MUNGU YAKUSAIDIE KISHA UFANYE MAAMUZI YAKO BINAFSI KUCHAGUA UPANDE WA KUSMAMIA IMANI YAKO. NAKUOMBEA SANA MUNGU AKUTIMIZIE HITAJI LA MOYO WAKO AMEN

1 comment:

  1. Yoctan Twesige PrudenceNovember 14, 2022 at 12:46 AM

    Dah!!Dunia inaelekea pabaya sasa

    ReplyDelete