Monday, December 5, 2022

TOP TEN (KUMI BORA) MASHIRIKA NA MAKAMPUNI BINAFSI YANAYOLIPA MISHAHARA MIKUBWA

 1. WALTER REED FOUNDATION

2. USAID PROJECTS

3. TBL
4. SBL
5.TCC
6. TWIGA CEMENT
7. SONGWE CEMENT
8. ALLIANCE ONE TOBACCO
9. COCA COLA
10. TOYOTA TANZANIA

Tuesday, November 29, 2022

President ajaye atoke Mbeya? Je nini maoni yako?

 Kama mjuavyo Mbeya ni kama Israel ya Tanzania, au Makkah kwa Waislamu! Vitu vingi vizuri na bora vinatoka Mbeya.

Kanisa la kwanza la kilokole lilianzia Ighale Mbeya, asilimia tisini na tisa ya wachungaji wenye upako na viwango wanatoka Mbeya, Maaskofu karibu robo tatu nchini wanatoka Mbeya, waimbaji wakubwa Tanzania wa dini wanatoka Mbeya ukianza na Daniel Mwasumbi, Efraim Mwansasu r.i.p, mpaka kizazi cha akina Boni Mwaitege wote wametoka Mbeya!

Mbeya ni mji mtakatifu sana kwa historia, ardhi yake imebarikiwa ni kama Denmark au Australia, muda wote ni kubichi. Watu wengi huwa wanashangaa uwingi wa makanisa Mbeya sababu ni kwamba Mbeya ndiyo Israel ya Tanzania, ni mji wa ibada.

Askofu Moses Kulola alianzia utume wake Itende Mbeya na Askofu Lazaro pia alilazimika kuanzia Mbeya kisha wakaicapture nchi kwa vuguvugu la wokovu!

Wasomi wanaotokea Mbeya ni material kwelikweli, kwa sasa iwe zamu ya Mbeya, Rais ajaye atoke Mbeya. Mtakuja kunishukuru hapa.

Haya NI maoni ya Mganguzi kutoka jamii forum

Sunday, November 13, 2022

CHUPI ZA UPAKO ZAWASHANGAZA WAKRISTO (Soma kisa hiki kikusaidie)

Jana nilimsindikiza shemeji  kwa nabii. Kilichompeleka yeye ni shida na changamoto za mahusiano yake. Mume mlevi, mume Malaya Kama mbwa, mume bahili, hajali ndoa Wala familia. Hajali ndugu zake Wala wa mkewe. Mume mgumu Kama ndevu za gaidi wa Mkuranga.

Rafiki yangu huyu aliniomba niandamane naye kwa nabii ili aniangalizie Mambo yangu, kwani tangu kipindi Cha Corona Biashara zangu zimeyumba Sana na hata shamba langu la nyoka  ambalo ndilo lilikuwa likiniingizia fedha za kigeni Sasa najihisi kana kwamba linaweza kunishinda kabisa ku operate.

Sasa kila mtu aliingia kwa awamu yake chumbani kwa nabii. Mimi ndiye niliyeanza na Kisha shem akafuatia. Nabii alikuwa mchangafu akanitia moyo kuwa hata kampuni kubwa Ulaya zimeanguka, nijipe Moto nitainuka Tena.

https://youtu.be/9VqdA0_DTNE

Akaniombea nikatoka, akaingia shemeji . huko ndani alikaa zaidi ya saa moja, akatoka nje akaniuliza una laki moja hapo unipe ntakurejeshea nyumbani? Nikamjibu cash Nina 75'000/ akasema nipe hizohizo, na Kama unayo balance kwenye simu rusha kwa namba hiii ya nabii. Nikamrushia.

Shem akaingia ndani ambako Sasa alikaa Kama dakika Saba Kisha akatoka nje. Safari ya kuelekea kwenye gari ikaanza, ndipo akaanza kunipa mchapo.

Nabii anatoa chupi za upako ambazo zinasaidia Kama mume hatulii, una ugumba etc. Chupi ni za Holland Wax na unaweza jipatia kwa kadiri utakavyo.

Bei ya kila moja ni laki unusu.

TAHADHARI :

Dada zangu sio kila nabii katoka kwa BWANA, muwe makini vinginevyo mtaibiwa sana

@Jr James (Facebook)

MIMI SITAKUPA USHAURI WOWOTE MSOMAJI WANGU BALI SOMA MANENO YA MUNGU YAKUSAIDIE KISHA UFANYE MAAMUZI YAKO BINAFSI KUCHAGUA UPANDE WA KUSMAMIA IMANI YAKO. NAKUOMBEA SANA MUNGU AKUTIMIZIE HITAJI LA MOYO WAKO AMEN

Tuesday, November 8, 2022

Zifahamu Nyimbo za Angela Chibalonza alizoimba kabla hajafahamika

Mwanamuziki WA nyimbo za Injili kutoka Congo aliyepata umaarufu mkubwa Sana miaka iliyopita aitwaye MAREHEMU Angela Chibalonza, aliwahi kuimba nyimbo KADHAA nzuri Sana kabla ya kufahamika kwenye Tasnia ya Muziki WA Injili.

  Mwanadada huyo ambaye Kwa sasa ni MAREHEMU aliimba nyimbo ZIFUATAZO ambazo NI miongoni MWA nyimbo ambazo yumkuni hukuwahi kuzifahamu. Nyimbo hizo zipo YouTube na mitandao mingine ya kidigitali ambapo nyimbo za Injili hupatikani.


Nyimbo hizo ni;

1. Inua Moyo wangu.  

    https://youtube.be/kuR5fjJZ8P8

2. Wamwendea (TENZI)

https://youtube.be/GFvfQCQhHtl

3. Ndio dhamana 

4. Tuonane bandarini (TENZI)

5. Yesu unipendaye (TENZI)

6. Mteteeni Yesu (TENZI)


Zipo Kwa mfumo WA video na audio ingia YouTube andika Angela Chibalonza na  utazipata nyimbo zake zote huko.

Edelea kubarikiwa na kuhudumiwa na taarifa mbalimbali za Gospo hapa kwenye blog yetu. 

Tunakupenda